Home » Maandalizi Nakuru Yakamilika Kwa Hafla Ya Rais Ruto

Maandalizi yamekamilika kwa Maombi ya Kitaifa ya Shukrani yatakayofanyika Jumapili katika Kaunti ya Nakuru.

 

Kulingana na Gavana Susan Kihika akizuru uwanja wa Riadha wa Nakuru ambapo maombi hayo yatafanyika, amesema sasa kila kitu kwa sasa ki tayari kwa hafla hiyo ambapo itaongozwa na Rais William Ruto pamoja na naibu wake Rigathi Gachagua.

 

Kihika amesema dhumuni la maombi hayo ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuwepo kwa amani katika kaunti mbalimbali kwa ujumla tangu kuapishwa kwake Rais ruto.

 

Hafla hiyo inatarajiwa kupambwa na Rais William Ruto ambaye ataongoza utawala wa Kenya Kwanza katika maombi hayo.

Kwa upande wake mbunge wa Gilgil Martha Wangari, amesema wanatarajia kuwa na takriban watu elfu 20,000 katika ibada hiyo ya maombi akisema itasaidia pakubwa kuweka taifa wakfu kwa Mungu.

Wangari ametoa wito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi na kutoa shukrani kwa umbali ambao taifa limefika, na pia kuombea ustawi.

Akitoa maoni sawa na hayo, Mbunge wa Nakuru Mjini Mashariki David Gikaria amesema kuna haja ya kutoa mwaliko huo kwa viongozi wa upinzani kwa vile ni tukio la kitaifa.

Kulingana na Gikaria, kunana haja ya kila mtu kuhudhuria akisema kuwa hiyo inaweza kusaidia katika kukomesha mikutano ya sasa inayoandaliwa na muungano wa Azimio.

 

Viongozi wengine waliohudhuria matayarishi hayo ni pamoja na Wabunge Samuel Gachobe wa (Subukia), Kuria Kimani wa (Molo), Paul Chebor wa (Rongai), Seneta wa Nakuru Tabitha Karanja, na Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti Liza Chelule miongoni mwa wengine.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!