Home » KNUT Yailaumu TSC Kwa Kuchelewesha Walimu Wa Junior Sekondari

KNUT Yailaumu TSC Kwa Kuchelewesha Walimu Wa Junior Sekondari

Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini (KNUT) kimeikashifu tume ya Huduma ya Walimu TSC kwa kuchelewesha kuwapeleka walimu katika Shule za junior Sekondari.

Katibu Mkuu wa KNUT Collins Oyuu, amesema hakuna mafunzo ambayo yamekuwa yakiendelea wiki moja baada ya wanafunzi wa Shule za Junior Sekondari kuripoti shuleni mwao na kuitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha vitabu vya ziada vinafikishwa shuleni kama ilivyoahidiwa na serikali.

Oyuu, aliyezungumza mjini Kisumu amedai ni walimu wachache waliripoti katika baadhi ya shule na wanatatizika kukabiliana na idadi kubwa ya wanafunzi.

Aidha, Oyuu ameitaka TSC kutoa barua za uhamisho wa walimu ili kuwawezesha kuhama kaunti zao.

 

Kulingana na Oyuu, barua za uhamisho tayari zimetumwa katika ofisi za TSC lakini viongozi hao bado hawajazitoa kwa walimu ili kuwawezesha kuhamia vituo vyao vipya.

 

Kadhalika, amesema walimu wametuma maombi mtandaoni ili kuhamishwa hadi vituo vipya kama ilivyoagizwa na TSC.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!