Home » Huduma Centres Kujengwa Katika Maeneo Bunge Yote

Huduma Centres Kujengwa Katika Maeneo Bunge Yote

Serikali itaanzisha vituo vya Huduma katika maeneo bunge yote, ndio usemi wake Katibu Mkuu wa Utumishi wa Umma Amos Gathecha.

 

Gathecha amesema hii itasogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza kuwa serikali inakusudia kuongeza huduma zinazotolewa kupitia vituo hivyo.

 

Aidha, amesema kwa sasa, kuna vituo 52 vya Huduma kote nchini na wanakusudia kuongeza idadi hiyo hadi 340. Akizungumza

 

katika ziara ya Kaunti ya Murang’a, Gathecha amesema wizara inashughulikia mpango mkuu wa kuanzishwa kwa vituo hivyo ili kuorodhesha gharama na kuongeza kuwa mradi huo utafadhiliwa na Benki ya Dunia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!