Rais Ruto Ajibu Madai Ya Mtoa Taarifa Wa IEBC
Rais William Ruto amejibu ripoti iliyotolewa na mtu anayedai kuwa mtoa taarifa wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) inayodai kuwa kura za 2022 Agosti zilivurugwa na kumpendelea yeye kushinda uchaguzi.
Mtoa taarifa huyo anadai zaidi kwamba kulikuwa na udanganyifu zaidi katika ngazi za maeneo bunge kwani matokeo mengi ya ubunge pia yaliibwa na kupendelea chama cha Rais Ruto cha UDA.
Charles Hornsby, mchanganuzi wa mara kwa mara wa siasa za Kenya aliweka ripoti hiyo chini ya uangalizi, akidai kuwa matokeo yaliyodaiwa yalichanganywa kutoka kwa matokeo rasmi na kubadilishwa ili kumpendelea Raila odinga.
Kauli ya Hornsby imeungwa na Rais williamRuto ambaye kwenye mtandao wa kijamii usiku a kuamkia leo amemsuta anayedaiwa kuwa mtoa taarifa akisema hakuna uwezekano kwamba Raila alimshinda Ruto katika maeneo yanayojulikana kuwa na wafuasi wengi wa Ruto na naibu wake.
Tangu kuibuka kwa ripoti za watoa taarifa, misukosuko imeonekana katika ulingo wa kisiasa huku serikali na upinzani zikijihusisha na mzozo wa maneno.
Rais Ruto ameshikilia kuwa hakuna kitakachomzuia kusimamia majukumu yake ya urais huku Raila kwa upande mwingine akitaka rais na naibu wake kujiuzulu.