Raila Atishia Kufichua Ziara Ya Siri Ya Chebukati
Kiongozi wa Azimio Raila Odinga sasa anadai kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Wafula Chebukati na makamishna wengine wawili walizuru nyumbani kwake kuzungumza naye licha ya kutoweka wazi ajenda walioyokuwa waliokusudia.
Raila ametoa changamoto kwa Chebukati na makamishna wa zamani Prof Abdi Guliye na Boya Molu kukanusha hadharani au kudhibitisha kwamba walizuru nyumbani kwake kabla ya kutangaza matokeo ya urais wa 2022 ili kupendelea rais William ruto.
Kiongozi wa upinzani pia alibainisha kuwa makamishna hao wa zamani walidai kuwa baadhi ya watu walijaribu kuwahonga.
Raila pia alidai kuwa watatu hao wa Chebukati pia walitembelea nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Mawaziri Raphael Tuju, wakisema ana ushahidi wa video.
Raila amemhimiza Rais Ruto akubali kwamba hakushinda uchaguzi wa urais wa Agosti 2022, hata kama alimkashifu Mkuu wa Nchi kwa kutoza ushuru mwingi nchini.
Aidha Raila aliwataka Wakenya kukataa ushuru unaoletwa na utawala wa rais Ruto, akisema lazima uidhinishwe na Bunge kabla ya kutozwa.
Hata hivyo alidai kuwa mapendekezo ya ubinafsishaji wa mali za umma yalikuwa na lengo la kumnufaisha Mkuu wa Nchi na wapambe wake serikalini.
Kiongozi huyo wa Azimio alijibu hatua ya mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) kuchunguza madai ya wizi wa kura katika uchaguzi wa 2022 na kusema kuwa ukweli unaweza kufichuka iwapo Azimio itaruhusiwa kuchunguza sava za Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Uhuru (IEBC).
Katika taarifa iliyoandikwa Januari 25, mkuu wa DCI Amin Mohamed alibainisha kuwa wamepokea malalamishi mengi kuhusiana na uchaguzi huo, na kuilaumu IEBC kwa kuendesha uchaguzi huo wenye dosari.
Kulingana na DCI inachunguza uhalali na uhalisi wa stakabadhi husika, akiitaka IEBC kutoa fomu 34-B ambazo zilitumika kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 2022.
Akihutubia kikao cha maombi huko Narok jana, Rais Ruto alisema hakuna mtu atakayempa idhini ya kutawala taifa Rais Ruto alidhibitisha kuwa uchaguzi wa Agosti 9 ulibainisha wazi mamlaka ya kila mrengo.
Licha ya dhana kuwa mikutano inayoendelea ya muungano wa Azimio huenda ikavuruga utendakazi wa utawala wake, Ruto alishikilia kuwa hatababaishwa.
Kwa upande wake Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka aliwataka wafuasi wao kudumisha amani kuendelea mbele.
Kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua upande wake alibainisha kuwa upinzani hautatishwa na serikali kuacha azma yake ya kupigania ushindi wao ulioibiwa.