Home » Wabunge Wasusia Kikao Mombasa Wakilalamikia NG-CDF

Wabunge Wasusia Kikao Mombasa Wakilalamikia NG-CDF

Kikao cha wiki moja cha bunge mjini Mombasa liligonga mwamba Jumatatu wakati wabunge walipoondoka katika shughuli za hoteli ya Pride Inn kupinga Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo bunge ya Serikali (NG-CDF) kucheleweshwa kutolewa.

Wabunge hao wametilia shaka kucheleweshwa kwa pesa hizo, wakisema kuwa shule zimefunguliwa, na kusababisha maelfu ya wazazi ambao wanategemea mpango huo kurundikana katika afisi zao.

Wabunge hao waliotaka kuhudhuria mkutano na Waziri wa Hazina Njuguna Ndungu wamependekeza kuwa pesa zilizotumiwa kufadhili makaazi yao zielekezwe kwa CDF.

Wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa Yatta Basil Ngui, wametaka fedha hizo zitolewe kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo ya wiki

moja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!