Watahiniwa 1,146 Wapata Alama Ya A
Jumla ya watahiniwa elfu 1,146 waliofanya mtihani wa KCSE mwaka jana walipata alama ya A.
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza matokeo ya mtihani wa KCSE katika Mitihani House, Nairobi, alisema kwamba….watahiniwa elfu 1,146 walipata alama ya A ikilinganishwa na elfu 1,138 katika mtihani wa mwaka wa 2021.
Mwaka 2022, jumla ya watahiniwa 841,416 walifanya mtihani wa KCSE, uliyofanywa kati ya Desemba 2 na Desemba 23.
Akizungumza katika ukumbi wa Mitihani House, waziri Machogu amebainisha kuwa serikali iliamua kutoa matokeo ya mitihani mapema ili kuwaruhusu wanafunzi hao kujiandaa kwa ajili ya mabadiliko ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
Machogu amewapongeza walimu na watahiniwa, akibainisha kuwa masomo 17 yalipata matokeo mazuri yaliyoimarika ikilinganishwa na masomo 11 mwaka wa 2021.
Machogu amesikitika kuwa mgomo ulioandaliwa katika Shule ya Wasichana ya St. Francis Mang’u ulikaribia kutatiza shughuli ya zoezi hilo.
Hata hivyo, ameapa kuwaongezea malipo na kushughulikia lalama zao.
Mtihani wa mwaka 2022 wavulana wamefanya vizuri zaidi huku waziri machogu akihimiza wasichana pia kujitahidi vilivyo.
Mbali na hayo wanafunzi pamoja na walimu kutoka shule mbalimbali wameendelea kutoa hisia zao kuhusiana na jinsi baadhi ya watoto wao walivyofaulu masomoni
Baadhi ya wakenya wanahisi hatua ya waziri wa elimu Ezekiel machogu kutotangaza shule zilizofanya vizuri kumepunguza joto miongoni mwa wanafunzi na walimu
kwa mujibu wa baadhi ya shule zilizofanya vizuri kama vile shule ya wavulana ya Kapsebet alikosoma Rais wa sasa William ruto wanadai kwamba matokeo ya leo yamekuwa ya ufanisi kwao kwani wanafunzi wengi kutoka shuleni humo watajiunga na vyuo vikuu.