Mashirika Kuchunguzwa Kudhibiti Ulaghai
Afisa mkuu wa jinsia katika kaunti ya Nakuru Gladys Kamuren, amesema ni sharti uchunguzi ufanyike dhidi ya shirika moja ambalo linadaiwa kuwatafutia wasichana ajira katika nchi ya Saudi Arabia kwenye eneo la Bahati.
Kamuren amesema uchunguzi utabaini iwapo shirika hilo limesajiliwa au lipo kinyume na sheria.
Wakati uo huo ametaka wasichana hao kuachiliwa na kurejeshewa stakabadhi zao kama vitambulisho.
Swala hili linajiri baada wasichana kutoka Pwani kufanya maandamano jana katika eneo la Bahati wakilalamikia kukandamizwa na kutorejeshewa stakabadhi zao.