Home » Mr Seed Atuhumiwa Kukimbia Jukumu La Kumlea Mwanawe

Mzazi mwenza wa msanii Mr Seed, Liz Sonia amemtuhumu msanii huyo kwa kukimbia majukumu ya kumlea mwanawe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Liz amesema Mr. Seed amekuwa akikwepa majukumu yake kama baba kwa kipindi cha miaka saba iliyopita.

Aidha amesema kitendo cha Hitmaker huyo wa “Dawa ya Barida” kushindwa kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wao ilimlazimu kujitolea kumhangaikia mwanawe ili aweze kukimu maisha yake.

Mrembo huyo amekiri kuchoshwa kubeba majukumu ya Mr. Seed ambaye amekuwa jeuri kwa muda mrefu huku akimuonya abadili mienendo yake vingnevyo atakuja kujutia siku za mbeleni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!