Home » TSC Yaidhinisha Uamisho Wa Walimu Wakuu Na Naibu Wao

TSC Yaidhinisha Uamisho Wa Walimu Wakuu Na Naibu Wao

Tume ya Kuajiri Waalimu nchini TSC imeidhinisha uhamisho wa waalimu 14,613 hadi kaunti zao za nyumbani, huku taasisi hiyo ya serikali ikihitimisha sera ya kuwatenganisha waalimu.

Ni Walimu 120 pekee ambao maombi yao ya uhamisho hayakutekelezwa kwa vile TSC bado haijapata mbadala wao.

Jumla ya walimu 14,733 kutoka kote nchini walikuwa wametuma maombi yao ya kuhamishwa hadi kaunti wanazotoka TSC ilipofungua dirisha hilo.

Kulingana na memo tuliopata, TSC itaendelea kutafuta nafasi kwa ajili ya uhamisho unaosubiri kabla ya maombi yaliyosalia kuidhinishwa.

Kutokana na takwimu, wakuu wa shule 226, naibu walimu wakuu 189 na walimu wakuu 1,948 wa shule za msingi walihamishwa hadi kaunti walizochagua.

Baadhi ya walimu 1,316 wa sekondari na walimu 10,934 wa shule za msingi watahamishwa katika mpango huo.

Tume hiyo ilifafanua kuwa wakuu wa mikoa wa TSC watasimamia uhamisho ndani ya mikoa yao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!