Mbuzi Gang! Yazidi kung’aa

Mbuzi Gang; Fathermoh, Joefes na iphoolish
Album ya kundi la muziki nchini, Mbuzi Gang “Three Wise Goats” inaendelea kubadilisha namba kila leo kwenye digital platforms mbalimbali.
Habari njema ni kwamba tayari imefikisha jumla ya Streams Milioni moja kwenye mtandao wa Boomplay ndani ya mwaka mmoja tangu itoke rasmi.
Album hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 13 moto moto, iliachiwa rasmi mwezi Januari mwaka 2022 ikiwa na kolabo 10 pekeake kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, Lava Lava, KRG The Don, Nina Roz, Katapilla, Ethic, Madini Classic, Naiboi na wengine kibao.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram Mbuzi Gang wamewashukuru mashabiki kwa upendo kwa kuandika, “1 million Streams on this masterpiece. Thank you fam. #3WG“
Ikumbukwe “Three Wise Goats” ni Album ya kwanza kwa kundi hili ambalo linaundwa na wasanii watatu ambao ni Fathermoh, Joefes na iphoolish