Home » Miili 37 Kutoka Kwa Ajali Ya Londiani Imetambuliwa

Miili 37 kati ya 52 ya waathiriwa wa ajali ya barabarani Ijumaa huko Londiani imetambuliwa.

 

Miili ambayo imehifadhiwa katika hospitali ndogo ya kaunti ya Londiani ilitambuliwa na jamaa za waathiriwa.

 

Kulingana na Msimamizi wa Matibabu wa hospitali ndogo ya kaunti ya Londiani Dkt Collins Kipkoech, miili 12 bado haijatambuliwa.
Kipkoech alisema miili ambayo imetambuliwa iliachiliwa kwa jamaa ili ihamishwe kwa kuhifadhiwa katika vyumba tofauti vya maiti wanavyotaka.

 

Alisema hospitali hiyo iko katika harakati za kupunguza msongamano wa chumba cha kuhifadhia maiti kwa kuweka miili ya ziada kwenye mashine ya kuhifadhia maiti ambayo ilitolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya.

 

Hifadhi ya maiti ya hospitali ndogo ya kaunti ina uwezo wa kubeba miili 16.

 

Kipkoech alifichua kuwa uchunguzi wa maiti zilizofanywa kwenye miili hiyo ulionyesha kuwa waathiriwa wengi walikufa kutokana na kiwewe kikubwa huku wengine wakinaswa na umeme.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!