Home » David Mwaure Aondolewa Katika Uongozi Wa Chama Cha Agano

David Mwaure Aondolewa Katika Uongozi Wa Chama Cha Agano

Msajili wa Vyama vya Kisiasa Anne Nderitu kubatilisha nafasi ya aliyekuwa mgombea urais wa 2022 David Mwaure kama kiongozi wa Chama cha Agano.

 

Katika notisi ya Gazeti, Nderitu alidokeza kuwa nafasi ya Mwaure itachukuliwa na Samuel Karanja.

 

Tangazo la Nderitu lilijiri siku chache baada ya wakili huyo kuteuliwa kuhudumu kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hazina ya Kitaifa ya Hifadhi ya Mazingira.

 

Zaidi ya hayo, msajili huyo alieleza kuwa mabadiliko hayo yalifanyika baada ya Mkutano Maalum wa Wajumbe wa Kitaifa (NDC) ulioitishwa na chama hicho.

 

Katika notisi hiyo, Wakenya waliopinga mabadiliko hayo walishauriwa kuwasilisha maoni yao kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP).

 

Japheth Koech alidumishwa kama naibu kiongozi wa Chama cha Agano.

 

Mwaure aliwania kiti cha urais bila mafanikio katika Uchaguzi Mkuu wa 2022. Alipata kura 31,987.

 

Kufuatia kushindwa kwake, babake mtangazaji wa BBC TV Waihiga Mwaura, aliahidi kuunga mkono serikali na hata kuomba wadhifa wa Spika wa Bunge la Kitaifa lakini akashindwa na Moses Wetangula.

 

Miezi kadhaa baada ya uchaguzi, Mwaura aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hazina ya Kitaifa ya Dhamana ya Mazingira kupitia notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mazingira Soipan Tuya.

 

Mwaure aliteuliwa katika bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

 

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi pia alibadilishwa kama kiongozi wa chama cha ANC baada ya kupata wadhifa wake mzuri serikalini Nafasi yake ilichukuliwa na Gavana wa Lamu Issa Timamy.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!