Home » Raila Odinga Awarai Wakenya Kutembea Kuelekea Kazini

Baada ya ujio wa Kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga humu nchini na kufululiza hadi katika uwanja wa Kamukunji, kiongozi huyo ameto wito kwa Wakenya kutokubali utawala wa Kenya kwanza ili kunyima Rais William Ruto mapato yanayohitajika kwa minajili ya uchumi.

 

Akipinga Ushuru wa Ongezeko la Thamani ya 16% ulioidhinishwa hivi majuzi kwa bidhaa za mafuta, Raila amewataka Wakenya kuepuka kutumia magari na kumnyima Ruto ushuru wa mafuta.

 

Kama sehemu ya uasi wa kiraia kunyima serikali ya Kenya ushuru wa mafuta, waziri mkuu huyo wa zamani amewataka Wakenya kuzingatia maoni yake na kuasi kutumia magari ambayo anasema bei ya mafuta imepanda hadi mara dufu na rais amekataa kushughulikia hali hiyo.

 

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii haswaa wafuasi wa azimio wamesuta utawala wa Kenya kwanza kwa kuwahadaa na kuwapea matumaini ya uongo ambapo wengi wamemsuta naibu rais Rigathi Gachagua ambaye ndiye kiongozi anayeendelea kuwakufisha moyo vijana wakenya wanaosaka ajira.

 

Katika mkutano huo Babu Owino mbunge wa embakassi mashariki vile vile alimsuta Gachagua kwa kauli ambayo anasema imewafanya wakenya kukata tama maishani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!