Eldoret: Mwanamke Atoweka Baada Ya Kudaiwa Kutupa Kijusi Kwenye Choo

Polisi mjini Eldoret wanamsaka msichana wa umri wa miaka 21 ambaye anashukiwa kutoa mimba na kutupa kijusi cha kiume cha miezi mitano ndani ya choo katika mtaa wa Munyaka.
Akithibitisha kisa hicho, David Sitati Wanyama amesema kijusi hicho kiligunduliwa na wakaazi wa eneo la Munyaka ambao waliwaarifu maafisa katika kituo cha polisi cha Kapsoya.
Wanyama amesema mshukiwa yuko mbioni na polisi wameanzisha msako katika eneo hilo.
Mwili wa kijusi hicho umepelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi kwa ajili ya kuhifadhiwa huku polisi wakiendelea na uchunguzi.