Home » Mahakama Kuu Kwa Mara Nyingine Yakataa Kusimamisha Mswada Wa Fedha

Mahakama Kuu Kwa Mara Nyingine Yakataa Kusimamisha Mswada Wa Fedha

Mahakama ya Juu kwa mara ya pili imekataa kusitisha Mswada wa Fedha ambao umetiwa saini na Rais William Ruto kuwa sheria leo asubuhi.

 

Jaji Mugure Thande wa Kitengo cha Kikatiba na Haki za Kibinadamu cha Milimani Hii leo Jumatatu, amekataa ombi la Seneta wa Busia Okiya Omtatah la kutoa maagizo ya muda dhidi ya utekelezwaji wa sheria hiyo.

 

Omtatah alitaka mahakama kusimamisha utekelezwaji wa sheria hiyo ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi la kikatiba la kupinga mchakato wa jinsi sheria hiyo ilivyotungwa.

 

Akiiomba mahakama hiyo kutoa amri za muda dhidi ya kutekelezwa kwa mswaada huo, Omtatah alipinga kuwa tangu awasilishe kesi hiyo Mei 31 mwaka huu, yeye na walalamishi wenzake walikuwa bado hawajapata wasikilizaji wa mahakama hiyo.

 

Pia aliomba kibali kwa mahakama kufanya marekebisho ya kesi hiyo kwa madai kuwa baadhi ya maombi yake yamepitwa na matukio.

 

Mwanasheria Mkuu Justin Muturi waziri wa Hazina Njuguna Ndung’u walipinga vikali kuidhinishwa kwa amri za muda zilizoombwa na Omtatah, wakisema kuwa wamewasilisha pingamizi la awali kupinga mamlaka ya mahakama kusikiza kesi hiyo.

 

Wakili wa Thande Kuria aliunga mkono maoni ya Ndung’u kwamba maagizo ya muda hayafai kutolewa hadi kuamuliwa kwa swali la iwapo mahakama ina mamlaka ya kusikiliza mzozo huo.

 

Katika kesi hiyo, Omtatah na wanaharakati wanne Eliud Matindi, Michael Otieno, Benson Odiwuor Otieno na Blair Angima Oigoro walipinga Mswada wa Fedha na kuutaja kuwa ni kinyume na katiba.

 

Walalamishi hao wanasema kuwa Mswada huo una vifungu 30 ambavyo vinakiuka Katiba kuhusu masuala ya ushuru.

 

Pia walitaka mahakama itambue kuwa kuna maswala muhimu ya kisheria yameibuliwa katika kesi hiyo na kupeleka kesi hiyo kwa Jaji Mkuu Martha Koome ili kujumlisha benchi ya majaji wasio na usawa kuamua kesi hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!