Barabara Ya Nairobi Express Kufungwa Kwa Muda Wikendi Hii
Barabara ya Nairobi Expressway itafungwa kwa muda wikendi hii ili kuandaa njia ya kuelekea Nairobi City Marathon.
Kampuni Moja ya Expressway, kupitia notisi ya umma iliyotolewa hii leo Jumatatu, ilisema barabara kuu itafungwa Jumamosi, Julai 1 saa 10 usiku, na itafunguliwa Jumapili, Julai 2 saa 4 jioni.
Mbio za Nairobi City Marathon ni hafla ya kila mwaka kwenye barabara kuu ya urefu wa kilomita 27 ambayo malengo yake huenda kusaidia jambo fulani.
Hili litakuwa toleo lake la pili.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mbio hizo za marathoni, mashindano ya mwaka huu yanahusu utunzaji wa mazingira, ambapo kwa kila kilomita moja itapandwa mti.