Home » Waziri Wa Afya Aapa Kuondoa Ufisadi KEMSA, NHIF

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha ameapa kuondoa ufisadi kutoka kwa Wakala wa Ugavi wa Dawa nchini (KEMSA) na Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF).

 

Anasema alidhamiria kukabiliana na makundi yenye nguvu na ushawishi mkubwa katika KEMSA na wizara kwa ujumla, ambao wanashirikiana na maafisa wa serikali walaghai kukomesha vita vinavyoendelea dhidi ya ufisadi katika mashirika hayo mawili kuu ya serikali.

 

Waziri huyo alizungumza akiwa Kitale ambako alisimamia uboreshaji wa Hospitali ya Misheni ya St. John Ambulance.

 

Pia aliwasilisha dawa za matibabu zenye thamani ya Ksh 330,000 kutoka KEMSA kwa kituo hicho.

 

KEMSA ndiyo kitovu cha kashfa ya mabilioni ya shilingi ambayo ilisababisha Mfuko wa Kimataifa wa Geneva kufutilia mbali zabuni ya Ksh 3.7 bilioni ya vyandarua vilivyotibiwa baada ya ripoti kwamba kampuni ya Uchina iliyokidhi mahitaji yote ya zabuni kutengwa isivyo haki.

 

 

Huku hayo yakijiri, NHIF, imekuwa ikikabiliwa na madai kwamba baadhi ya maafisa wake wanatumia hospitali mbovu kukamua kwa mikataba ya kashfa, ikiwa ni pamoja na kulaghai hazina hiyo kwa kutoa upasuaji usio wa lazima na unaoweza kuwadhuru Wakenya wazee.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!