Home » Wakaazi Wa Vihiga Wataka Kanisa La Mackenzi Kufungwa

Wakazi katika Kaunti ya Vihiga wameambia Kamati ya ADHOC inayochunguza vifo vya Shakahola kuzima kanisa Goodnews International Church

 

Wanasema serikali imechelewa kulifunga kanisa hilo licha ya kisa hicho cha kutisha ambacho kimesababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

 

Hata hivyo, katika dokezo ilo hilo, naibu kamishna wa kaunti ya Vihiga Florence Sitawa alisema katiba ya Makanisa ndiyo sababu kuu inayofanya machafuko yazuke makanisani.

 

Kamati ya dharura ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Seneta Shakila Abdallah pamoja walifika katika Kaunti ya Vihiga kukutana na familia ambazo jamaa zao walifariki katika msitu wa Shakahola.

 

Kamati hiyo ilipokelewa na Gavana Ottichilo na Seneta Godfrey Osotsi.

 

Osotsi alisema serikali inapaswa kuwajibika kwa tukio la Shakahola.

 

“Serikali ilikuwa wapi wakati Paul Mackenzi alipokuwa akihimiza watu kufa kwa njaa,” Osotsi aliuliza.

 

“Watu waliingizwa kwenye fujo hii ya Mackenzi kutokana na umaskini na serikali lazima itafute njia ya kuboresha maisha ya watu,” aliongeza.
Osotsi alisema ikiwa uchumi wa Kenya utadorora zaidi, Wakenya wengi zaidi wataendelea kuitwa na wahubiri wahuni.

 

Alibainisha kuwa kuwa na sheria zinazoongoza kanisa si jambo zuri, akisema makanisa yana sheria zao zinazopaswa kuheshimiwa na kuachwa.

 

“Kama tuna kanuni, zinapaswa kuwa za makanisa lakini sio Sheria ya Bunge,” alisema.

 

Ottichilo aliambia kamati ya muda ya Seneti kwamba makanisa ndani ya kaunti ndio chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama.
Alisema mabishano ndani ya makanisa hayo yamesababisha hata vifo.

 

Kamati ya Seneti kwa sasa inachunguza kuenea kwa mashirika ya kidini na hali inayosababisha vifo.

 

Kamati imekuwa Malindi, Nairobi, Kisumu na kwa sasa katika kaunti ya Vihiga.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!