Home » Waziri Nakhumicha: Wakenya Watapata Thamani Ya Pesa Zao Kupitia NHIF

Waziri Nakhumicha: Wakenya Watapata Thamani Ya Pesa Zao Kupitia NHIF

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha anasema hatakata tamaa katika dhamira yake ya kuona kuwa mabadiliko yanafanywa katika Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF).

 

Haya yanajiri huku uchunguzi kuhusu madai kwamba baadhi ya taasisi za afya za kibinafsi zilizojihusisha na udanganyifu kwa kuwasilisha madai ya uwongo ya matibabu bado unaendelea.

 

Akizungumza jana Ijumaa wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Moyo na Kitengo cha Cath Lab katika Hospitali ya Coptic, Nakhumicha alisema kuwa mabadiliko kutoka Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) hadi hazina ya bima ya afya ya jamii ambayo inaendelea, itahakikisha Wakenya kupata thamani ya pesa zao.

 

Alidokeza kuwa mgonjwa aliyeibua madai hyo atatunzwa na mfuko wa bima ya afya NHIF bila kujali atachagua kwenda hospitali ya kibinafsi au ya umma.

 

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha Jumatatu aliwasimamisha kazi mameneja wa tawi la Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Hospitali (NHIF) wanaodaiwa kuwalaghai Wakenya.

 

Kusimamishwa kazi kwa maafisa hao kulifuatia ufichuzi wa NTV uliofichua watu walaghai wanaojifanya wahudumu wa afya wanaohusishwa na NHIF.

 

Ufichuzi huo uliangazia vitendo vyao vya udanganyifu, ambavyo vililenga wakaazi wa Meru na Nairobi kwa kutoa ahadi za uwongo ili kupunguza athari za kudhoofisha za arthritis.

 

Kwa hivyo, Nakhumicha ameagiza Baraza la Madaktari na Madaktari wa Meno la Kenya, pamoja na Bodi ya Dawa na Sumu, kuanzisha uchunguzi huru kuhusu suala hilo.

 

Kusudi lao kuu ni kufichua utovu wowote wa nidhamu au ukiukwaji wowote, kwa lengo la kusaidia katika kutambua waliohusika.
Waziri huyo alitoa agizo la ziada kwa bodi ya NHIF, akiwaagiza waanzishe uchunguzi kuhusu visa hivyo vya ulaghai na wampe ripoti kufikia Jumatano.

 

Kwa kuzingatia ufichuzi huo wa kushangaza, Nakhumicha pia alitangaza kwamba watafanya ukaguzi wa kina wa mtindo wa maisha kwa wafanyikazi wote wa NHIF.

 

Nakhumicha pia amefahamisha Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusu uchunguzi huo, na wameratibiwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mpango huo wa kustaajabisha wa udanganyifu.

 

Wakati uo huo ameagiza kwamba hospitali zilizoathiriwa za Meru na Nairobi zinapaswa kuhamishia wagonjwa wao kwenye vituo mbadala “Kwa maslahi ya usalama wa mgonjwa na utunzaji usiokatizwa”.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!