Home » Familia Ya WaJesus Kuchukua Hatua Dhidi Ya Watu Wanaochafua Chapa Yao

Familia Ya WaJesus Kuchukua Hatua Dhidi Ya Watu Wanaochafua Chapa Yao

Content creators nchini Kenya Milly WaJesus na Kabi WaJesu wamefichua kuwa watachukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote anayekashifu na kuchafua chapa zao na jina la familia.

 

Wakizungumza kwenye chaneli yao ya YouTube, Familia ya WaJesu ilisema inauma watu wanapotengeneza chaneli ili tu kuwatusi na kukashifu chapa ambayo wamejitahidi sana kuijenga.

 

Haya yalijiri baada ya video ya Kabi WaJesu akicheza ngoma na mama mkwe Bi Ng’ang’a kusambaa.

 

Baadhi ya watayarishi walitengeneza maudhui kwenye video hiyo huku wengine Wakimtuhumu mama yake Milly kwa kumroga Kabi.

 

Bi Ng’ang’a alieleza kuwa Kabi ni mwanawe na inamtia uchungu watu wanapomshtumu kwa mambo mabaya kwa sababu tu yuko karibu na watoto wake.

 

Kabi alibainisha kuwa baadhi ya watu wamepakia video kwenye chaneli zao za YouTube wakiichafua familia ya WaJesu na mama mkwe wake, na kusahau kuwa yeye ni mama na si mwigizaji.

 

Familia hiyo ilifichua kuwa yeyote ambaye anahisi kuwachafua na kumtusi mamake Milly hatashughulikiwa katika sehemu ya maoni bali atalazimika kulipa kwani chapa yao, WaJesu ndiyo inayowaingizia pesa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!