Home » Ushirikiano Wa Sekta Ya Umma Na Binafsi Wazindua Mpango Wa M-mama

Ushirikiano Wa Sekta Ya Umma Na Binafsi Wazindua Mpango Wa M-mama

Serikali ya Kenya na ile ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Vodafone na Mpesa Foundation imeingia katika mkataba kati ya sekta ya umma na binafsi kwa lengo la kuboresha sekta ya afya.

 

Hatua hiyo imefanikisha kuundwa kwa mpango wa M-mama ambao utasaidia katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika kaunti.

 

Mpango wa M-mama ni mfumo wa rufaa wa dharura ambao husafirisha kwa haraka wanawake wajawazito na watoto wachanga wanaokabiliwa na matatizo hadi kwenye vituo vya afya vinavyofaa.

 

Anne Waiguru, Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, alisema wakati wa tangazo la mpango huo kwamba itahakikisha kuwa hakuna mama atakayefariki wakati akijifungua.

 

Waiguru alisema kuwa mpango wa M-Mama ni nyongeza ya kukaribisha kwa ushirikiano ambao uko mstari wa mbele katika mipango ya afya ya uzazi na mtoto nchini Kenya.

 

Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Afya Susan Nakhumicha alisema kuwa ushirikiano wa M-Mama unawiana na ajenda ya maendeleo na afya ya Kenya na utatoa fursa ya kuimarisha huduma ya afya ya msingi na kuweka sekta ya afya kwenye dijitali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!