Home » Mvuvi Auawa Na Kiboko Katika Ziwa Victoria

Mwanamume mwenye umri wa miaka 48 ameuawa na kiboko huku mwingine akipata majeraha mabaya karibu na ufuo wa Lwanda eneo bunge la Suba Kaskazini, kaunti ya Homa Bay Jumatano asubuhi.

 

Mvuvi huyo aliyetambulika kwa jina la Janes Okombo alifariki papo hapo katika tukio hilo la saa 5 asubuhi alipokuwa akivua samaki katika Ziwa Victoria.

 

Inaarifiwa Okombo aliondoka nyumbani akiwa na mwenzake aliyetambulika kwa jina la Gilbert Abich, hata hivyo, wakiwa njiani kuelekea eneo la uvuvi, walikutana na kiboko ambaye aliwavamia.

 

Kiboko huyo aligonga mashua yao, na baada ya kupinduka, iliwashika na kumng’ata Gilbert kabla ya kumuua Okombo.

 

Mwenyekiti wa Mtandao wa Usimamizi wa Ufuo wa Kaunti ya Homa Bay Edward Oremo anasema wavuvi hao walikosa msaada baada ya kiboko huyo kuvunja mashua yao.

 

Kikosi kinachojumuisha Huduma ya Wanyamapori wa Kenya (KWS), maafisa wa Huduma ya Walinzi wa Pwani ya Kenya, wavuvi na wakaazi wamepiga kambi katika ufuo wa ziwa kuanza kuuchukua mwili wa Okombo.

 

Wakati uo huo, Gilbert alikimbizwa katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Mbita kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay ili kupata dawa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!