Home » Kizaazaa Chaibuka Murang’a

Kizaazaa kilitanda nje ya Bunge la Kaunti ya Murang’a huku wabunge kadhaa wakizuia lango la wawakilishi wadi dhidi ya kutoka nje ya makao ya bunge la kaunti.

 

Mbunge wa Maragua Mary Waithira, mwakilishi wa wanawake wa Murang’a Betty Maina, Beatrice Elachi wa Dagoretti Mashariki na Seneta mteule Veronica Maina walikuwa wamekita kambi langoni wakipinga kusimamishwa kazi kwa Grace Nduta, mwakilishi wa wadi ya Kanyenyaini.

 

Mzozo huo ilianza wakati wawakilishi wadi waliokuwa ndani ya Bunge walipomaliza kikao chao na kutaka kuondoka.

 

Wawakilishi hao waliingia kwenye magari yao na kuanza kupiga kelele wakiwataka wabunge waondoke njiani.

 

Juhudi za maafisa wa polisi na maafisa wa usalama katika Bunge la Kaunti ya Murang’a kudhibiti pande hizo mbili ziliambulia patupu huku kila mmoja akimshtaki mwenzake.

 

Waithira alisisitiza kuwa wawakilishi hao wanapaswa kusalia nyuma na kuwasikiliza kwa sababu ujumbe huo ulielekezwa kwao.

 

Mbunge huyo pia alishangaa ni kwa nini polisi walikuwa wametumwa katika bunge hilo akisema hawakuwa na nia ya kuvamia ndani ya bunge.

 

Maina kwa upande wake alisema polisi wanapaswa kuzingatia kukabiliana na wahalifu badala ya kupiga kambi katika uwanja wa bunge bila kufanya lolote.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!