Home » MahakamaYa Juu Yaondoa Kesi Ya Itumbi Dhidi Ya Serikali

MahakamaYa Juu Yaondoa Kesi Ya Itumbi Dhidi Ya Serikali

Mahakama ya juu imeondoa kesi ambayo ilikuwa imewasilishwa na Katibu Mkuu wa Utawala wa mawasiliano na teknolojia ICT (CAS) Dennis Itumbi dhidi ya serikali kuhusu kesi ya mauaji .

 

Itumbi kupitia kwa wakili Georgiadis Majimbo aliambia mahakama kuwa kesi ya jinai iliyokuwa mbele ya mahakama ya chini iliondolewa, kwa hivyo, ingefaa kesi hiyo iondolewe katika mahakama kuu.

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mashtaka hawakupinga maombi hayo.

 

Wiki iliyopita mahakama ya Nairobi iliwaachilia Itumbi na mshitakiwa mwenzake Samuel Gateri kutokana na mashtaka ya uhalifu.
Mahakama ilibaini kuwa sehemu ambayo wawili hao walishtakiwa ilikuwa kinyume na katiba.

 

Wawili hao walikuwa wamejitetea kwa madai ya kughushi barua iliyotaja kwamba afisa mkuu wa serikali katika utawala wa Rais wa zamani Uhuru Kenyatta alipanga njama ya kumuua Naibu Rais wakati huo, ambaye sasa ni Mkuu wa Nchi.

 

Mpango huo wa mauaji ulisemekana kutokea katika hoteli ya La Mada.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!