Baadhi Ya Wanachama Wataka Ruto Kupatana Na Seth Panyako

A collage of President Ruto and Seth Panyako
Baadhi ya wanachama wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kutoka Kaunti ya Kakamega wamemtaka kiongozi wa chama chao Rais William Ruto kupatana na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Seth Panyako.
Kulingana na wanachama hao, Panyako, ambaye alijiuzulu kutoka wadhifa wa chama hicho mwezi Mei, ndiyo sababu ya UDA kupata umaarufu katika Kaunti ya Kakamega.
Mwanachama mwingine, Arnold Shisanya alionya kwamba umaarufu wa UDA huko Kakamega huenda ukashuka ikiwa Rais hatapatana na katibu mkuu wa Kenya Union of Nurses.
Wanachama wengine wa chama hicho walimtaka Katibu Mkuu wa UDA, Cleophas Malala kupatanisha pande hizo mbili.
Panyako alitaja msimamo wake kuhusu Mswada wa Fedha wa 2023 kama sababu ya kutofautiana kwake na mkuu wa chama cha UDA, rais Ruto.