Home » Kamati Ya Bunge Yapendekeza Ushuru Wa Nyumba Kupunguzwa

Kamati Ya Bunge Yapendekeza Ushuru Wa Nyumba Kupunguzwa

Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Fedha na Mipango imetoa mapendekezo zaidi kwa vifungu kadhaa vyenye utata katika muswada wa fedha wa 2023, kabla ya kuwasilishwa kwake Bungeni kesho Jumanne.

 

Katika orodha hiyo ni pendekezo la kupunguza asilimia 3 ya Ushuru wa Nyumba hadi asilimia 1.5 na kukatwa tu kutoka kwa wafanyikazi wa umma pekee.

 

Kamati vile vile imependekeza utekelezwaji wake pia uahirishwe hadi Januari 2024 ili kuweka mfumo wa kisheria wa kuzuia mvutano kabla ya utekelezaji wake.

 

Ushuru ulikuwa jambo kuu la mazungumzo katika Mswada wa Sheria ya Fedha wa 2023 wa kusikilizwa kwa ushiriki wa umma.

 

Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Molo Kuria Kimani amesema pia wanapendekeza kwamba asilimia 15 ya V.A.T kwenye Uundaji wa Maudhui ya Dijitali ipunguzwe hadi asilimia 5.

 

Kamati pia imependekeza msamaha wa kodi kwenye pembejeo za Kilimo, chanjo na magari ya umeme.

 

Hata hivyo, Kamati ya Fedha ya Bunge la Kitaifa imependekeza kubakishwa kwa VAT ya asilimia 16 kwenye bidhaa za Petroli.

 

Huku Mswada wa Fedha wa 2023 ukipangwa Kuwasilishwa bungeni kesho Jumanne, mswada huo kusomwa mara ya pili kwenye sakafu ya baraza hilo unatarajiwa Jumatano baada ya kuidhinishwa na Kamati ya Biashara ya Bunge.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!