Home » Gavana Sakaja Azindua Mpango Wa Chakula Kwa Shule Za Msingi

Gavana Sakaja Azindua Mpango Wa Chakula Kwa Shule Za Msingi

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, Alhamisi, amepiga hatua muhimu katika kutimiza ahadi yake ya kampeni kwa kuzindua mpango wa chakula cha bure katika shule za msingi.

 

Sakaja alitangaza kuwa shule zilizotengwa kwa ajili ya programu hiyo zitafurahia milo ya bure kuanzia muhula wa tatu wa mwaka huu.

 

Kwa mujibu wa kalenda ya shule, muhula wa tatu unaanza Septemba hadi Desemba, kulingana na ratiba ya mitihani ya kitaifa.

 

Kaunti ya Nairobi itafadhili mpango wa chakula bila malipo kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa.Gavana huyo ametangaza hayo kufuatia mkutano na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, Makatibu Wakuu Belio Kipsang, na Beatrice Inyangala.

 

Wizara ya Elimu iliapa kumuunga mkono Sakaja katika kuharakisha mpango huo wa kuzifikia shule mbalimbali za msingi ndani ya jiji hilo.

 

Ili kufanikisha mpango wa kulisha shuleni, Sakaja alitangaza mipango ya kujenga jikoni kuu ili kusambaza chakula kwa shule za umma.

 

Jumatatu, Juni 5, gavana huyo wa mara ya kwanza alishiriki kisiri katika jiko kubwa zaidi barani Afrika analojenga Nairobi ili kutimiza ahadi hiyo.

 

Sakaja alishirikiana na shirika lisilo la faida la Food for Education, kujenga jiko hilo.

 

Kando na mpango wa chakula cha bure, Sakaja alifichua kuwa kaunti yake ilikuwa inafikiria kutenga ardhi kwa upanuzi wa shule na vituo vingine vya ufundi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!