Home » Kifo Cha Jeff Mwathi Kutajwa Tena Agosti

Uchunguzi wa kifo cha Jeff Mwathi, aliyefariki Februari mwaka huu nyumbani kwa DJ Faxto na kuzikwa kaunti ya Nakuru sasa utafanyika Agosti 10.

 

Kesi hiyo imejadiliwa mbele ya Hakimu Zainab Abdul hii leo Alhamisi, ambaye amemuagiza afisa wa upelelezi kutoa nyaraka atakazotumia katika uchunguzi huo kwa pande zinazohusika.

 

Takriban mashahidi 35 wataitwa kuangazia kifo cha Mwathi.

 

Anne Mwathi, mamake marehemu Mwathi, ambaye alikuwepo mahakamani hii leo Alhamisi, ameambia vyombo vya habari kuwa familia yake imekuwa na uchungu tangu Mwathi alipofariki.

 

DJ Fatxo, ambaye nyumba yake inasemekana Mwathi alifarikia hadi sasa imefungwa baada ya ushahidi kushindwa kumhusisha na kifo hicho.

 

Kifo hicho kilizua gadhabu ya umma baada ya kufichuliwa kuwa marehemu mbunifu wa mambo ya ndani alikufa baada ya sherehe za usiku.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!