Home » Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta Apata Pigo Jingine

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amepata pigo lingine baada ya kesi iliyowasilishwa na katibu mkuu Jeremiah Kioni kuhusu mzozo wa chama cha Jubilee kutupiliwa mbali.

 

Katika uamuzi uliotolewa ,kamati ya utatuzi wa migogoro ya ndani (IDRC) imethibitisha kuwa Nelson Dzuiya na Joshua Kutuny waliotajwa kama waasi wa chama hawakukiuka sheria kwa kuitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

 

Katika kufikia uamuzi huo, Kamati inayoongozwa na Gideon Solonka imebaini kuwa mlalamishi ameshindwa kuitisha kikao cha NEC kama ilivyoamuliwa na kamati ya usimamizi ya taifa na kusababisha washtakiwa kuingilia kati.

 

Kamati imeeleza kuwa mlalamishi alikiuka wajibu wake wa uadilifu kwa kushindwa kuitisha kikao chochote cha NEC.

 

Kioni aliwasilisha malalamiko hayo Mei 18 akitaka kutangaza maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha NEC kuwa ni kinyume cha sheria.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!