Home » Wasioamini Mungu Wasema Mkutano Wa Maombi Ya Ni Dharau Kwa Wakenya

Wasioamini Mungu Wasema Mkutano Wa Maombi Ya Ni Dharau Kwa Wakenya

Wafuasi wasioamini uwepo wa Mungu “Atheists“ wamekashifu mkutano wa Maombi uliofanyika leo Nairobi kule safari park hotel wakisema ni ufujaji wa pesa za walipa ushuru na dharau kwa ‘Wakenya wanaohangaika’ kwa uchumi unaowatesa kila siku.

 

Katika taarifa kupitia shirika lao la Atheists in Kenya Society, wameikafu serikali ya Kenya Kwanza wakisema “serikali inapaswa kupata vipaumbele vyake ” na wala si kukejeli wakenya kwa kufanya maombi na wakazi wengine wanalala njaa.

 

“Serikali ya Kenya Kwanza iliingia mamlakani kwa ahadi ya kubuni nafasi za kazi na kukabiliana na gharama ya juu ya maisha.

 

Takriban mwaka mmoja tangu utawala wa William Ruto uingie mamlakani, mamilioni ya Wakenya wamesalia bila kazi au kuajiriwa duni. Gharama ya bidhaa za kimsingi bado haiwezi kumudu Wakenya wengi,” rais wa jumuiya hiyo, Harrison Mumia alisema kwenye taarifa.
Mumia pia ametoa wito kwa mkutano wa ya kitaifa Maombi ulioratibiwa kufanyika kila mwaka ukomeshwe.

 

Rais Ruto aliongoza mamia ya viongozi na wageni katika maombi ya mwaka huu katika Hoteli ya Safari Park yenye mada kuhusu maridhiano.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!