Home » Azimio Yasuta Kenya Kwanza

Mshirikishi mkuu wa muungano wa Azimio La Umoja One-Kenya Martha Karua amezungumzia dhidi ya kile anachokiita udhalilishaji wa serikali ya Kenya Kwanza dhidi ya Rais mstaafu mwenyekiti wa Azimio Uhuru Kenyatta.

 

Akihutubia wanahabari jijini Nairobi hii leo Jumatatu, Karua amesema mizozo ya uongozi iliyoshuhudiwa katika Chama cha Jubilee katika wiki za hivi majuzi imepangwa ili kumdharau rais huyo wa zamani na kuleta mgogoro katika eneo lenye kura nyingi za Mlima Kenya.

 

Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni, ambaye pia alikuwa kwenye kikao hicho ametoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi dhidi ya Kenyatta, ambayo aliyataja kuwa hayafai.

 

Malumbano katika Jubilee yalimfanya Kenyatta kuitisha Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) mwezi uliopita ambalo Kamati ya Kusuluhisha Mizozo ya Ndani ya chama (IDRC) hata hivyo imetupilia mbali na kusema kuwa ni batili.

 

Kenyatta aliongoza Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) la mrengo wa Kioni unaoongozwa na Jubilee mnamo Mei 22 huku kukiwa na kampeni ya kuwatimua wanachama walioasi.

 

Chama cha Jubilee kilikuwa kimekumbwa na mizozo ya uongozi baada ya mrengo unaoongozwa na Kanini Kega kufanya mabadiliko ya uongozi ambayo yalipelekea Kenyatta kuondolewa kama kiongozi wa chama, Seneta Mteule Sabina Chege akiteuliwa kama kaimu kiongozi wa chama huku Kega akichukua nafasi ya Kioni kama Seneta.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!