Home » Mashirika Ya Kiraia Yapinga Mswada Wa Fedha 2023

Mashirika ya kiraia yamepinga mswada uliowasilishwa bungeni wa kutaka kufuta sheria katika Sheria ya Kupambana na Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi ambayo inawazuia maafisa wa umma kujihusisha na ufisadi.

 

Mswada huo wa marekebisho ambao unafadhiliwa na Mbunge wa Mbeere Kaskazini Geoffrey Ruku Kariuki, unalenga kuwaepusha maafisa wa umma dhidi ya uhalifu ikiwa watakosa kufuata miongozo ya ununuzi na utekelezaji wa miradi ambayo haijapangwa.

 

Mashirika hayo, miongoni mwao ni Transparency International (TI), Mzalendo, Muungano wa Katiba na Mageuzi ya Elimu (CRECO), ECOR na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC), yameteta kuwa marekebisho yaliyopendekezwa yatabatilisha mafanikio ambayo nchi imechukua kukabiliana na ufisadi.

 

Wameliomba bunge kupitia Kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria (JLAC) kupuuza mapendekezo hayo.

 

Mbunge Kariuki anataka vifungu vya 2(b) na 2(c) vifutwe katika Kifungu cha 5 cha Sheria ya Kupambana na Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi ambacho kinaelekeza kwamba afisa au mtu ambaye majukumu yake yanahusu utawala, ulezi, usimamizi, upokeaji au matumizi ya kitu chochote.

 

Kuhusu Mswada wa Fedha wa 2023, makundi ya washawishi yamemkashifu Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhusu matamshi aliyotoa kuwa mswada huo utaidhinishwa bungeni licha ya maandamano ya watu fulani.

 

Wanasema matamshi ya naibu rais Gachagua hayakufaa, haswa wakati huu ambapo Wakenya wanakabiliana na uchumi unaoporomoka.
Ili kuhakikisha mswada huo unasambaratika Bungeni, wamesisitiza kuwa wataweka shinikizo kwa wabunge kuukataa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!