Mwanaume Aliyefungwa Kimakosa Aachiliwa Baada Ya Kifungo Cha Miaka 10
Mwanamume aliyefungwa maisha baada ya kushtakiwa kwa wizi wa kutumia nguvu amepata afueni baada ya mahakama ya rufaa kumwachilia huru.
Mahakama iligundua kuwa mshtakiwa, Stanley Njeru Kira ambaye tayari alikuwa ametumikia kifungo cha miaka 10 alikamatwa kimakosa baada ya umma kumshutumu kuwa mhusika katika kisa cha wizi kilichotokea Naivasha kaunti ya Nakuru.
Katika kisa hicho kilichotokea mwaka wa 2010, Njeru alishtakiwa kwa kumwibia dereva teksi gari aina ya Nissan Sunny station Wagon Ksh6,500.
Wakati huo, mwathiriwa aliwaambia polisi kwamba alikuwa akielekea katika kambi ya wakimbizi wa ndani I.D.P akiwa na wanaume wawili waliokuwa wamemkodi kuwasaidia kumchukua mwanamke katika eneo hiloHata hivyo, walipofika huko mwanamke huyo hakuonekana.
Aidha mwanamume anayedai kuwa Njeru alijitolea kuwasaidia kumpata mwanamke aliyetajwa hapo awali Takriban kilomita 4 baadaye, mwanamume waliyemruhusu kuingia ndani ya gari alimnyonga dereva kwa kamba na kumwamuru asimamishe gari.
Baadaye wakati wa mchana, alitoa tahadhari kwa umma na kuwafanya watu hao watatu kutafuta usalama baada ya kundi la watu wenye ghadhabu kuanza kuwatafuta.
Njeru alikamatwa na umati huo alipokuwa akihama eneo hilo.
Akiwa mbele ya majaji Fatma Sichale, Lydia Achode na Weldon Korir mahakama iligundua kuwa shahidi aliyemkamata Njeru hakumwona akitoka kwenye gari hilo.
Mshtakiwa hata hivyo amesisitiza kuwa hakuhusika katika wizi huo.