Home » Ubalozi Wa Marekani Wahairisha Tarehe Ya Kuanza Kwa Ada Mpya Za Visa Za Wahamiaji

Ubalozi Wa Marekani Wahairisha Tarehe Ya Kuanza Kwa Ada Mpya Za Visa Za Wahamiaji

Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi Hii leo Ijumaa, Juni 2, uliahirisha mipango ya kuongeza ada za viza kwa waombaji wasio wakazi rasmi.
Katika notisi, ubalozi ulitangaza kuwa malipo hayo mapya yataanza Jumamosi, Juni 17.

 

Utawala wa Rais Joe Biden uliongeza tarehe ya kuanza kwa siku 18. Hapo awali, malipo mapya kwa wasio wahamiaji mahususi yalitakiwa kuanza kutekelezwa Jumanne, Mei 30.

 

Ubalozi huo haukuchapisha mara moja sababu za kuahirisha ada za visa.

 

Miongoni mwa walioathiriwa na mabadiliko yaliyochapishwa Jumatano, Mei 3, ni pamoja na, wafanyikazi wa muda, wanafunzi, watalii na wawekezaji.

 

Kwa mujibu wa sera ya kigeni ya Rais Biden, Marekani iliongeza ada za visa kwa wanafunzi na watalii kutoka Ksh21,800 hadi Ksh25,206 (USD160 hadi USD185).

 

Kuanzia Jumamosi, Juni 17, wafanyikazi wa muda wataanza kulipa Ksh27,931 kutoka Ksh25,887 ili kupata visa vyao vya kusafiri.

 

Wawekezaji ndio walioathirika zaidi kwani serikali ya Marekani ilipandisha ada ya viza kwa Ksh15,000. Ili kupata hati hiyo muhimu ya kusafiri, lazima wawe na Ksh42,918 katika mabadiliko. Hapo awali, wawekezaji wa mkataba walikuwa wakilipa Ksh27,931 kupata visa vyao.

 

“Watu ambao tayari wamelipa ada iliyopo, ya chini (ya Non-Immigrant Visa) ya NIV hawatalazimika kulipa tofauti hiyo mara tu ada inapoongezeka mnamo Mei 30, 2023. Malipo yote ya ada ya NIV yaliyofanywa mnamo au baada ya Oktoba 1, 2022, ni halali kwa siku 365,” Ubalozi wa Marekani ulisema.

 

“Risiti za ada za NIV zilizolipwa kabla ya Oktoba 1, 2022, zitaendelea kuwa halali hadi Septemba 30, 2023,” ilifafanua zaidi.

 

Ongezeko hilo la ada linatokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji kulikosababishwa na mfumuko wa bei duniani. Ubalozi, hata hivyo, umeapa kuharakisha muda wa visa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!