Home » Nakuru: Mshukiwa Mmoja Akamatwa Polisi Wakinasa Pombe Haramu

Maafisa wa polisi katika eneo la Naivasha kaunti ya Nakuru wamemkamata mshukiwa mmoja kuhusiana na biashara za pombe haramu.

 

Buleti Amson mwenye umri wa miaka 20 alikamatwa wakati wa operesheni ambapo masanduku 46 ya pombe haramu yalitwaliwa pamoja na bidhaa nyingine haramu za kutengenezea na kupakia pombe hiyo katika chupa mbalimbali.

 

Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS), katika taarifa hii leo Alhamisi, imesema hatua za dharura za maafisa na mashirika mengi walivamia majengo ya Naivasha na kufanikiwa kupata bidhaa hizo.

 

Idara ya polisi imesema pia kwamba stika za Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) pia zilipatikana wakati wa uvamizi huo.

 

Mshukiwa huyo atafikishwa mahakamani siku ya Ijumaa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!