Home » Madaraka Day: Wawakilishi Wa Wadi Wa Embu Wasitisha Vikao

Madaraka Day: Wawakilishi Wa Wadi Wa Embu Wasitisha Vikao

Wawakilishi wadi wa bunge la kaunti la Embu wamesitisha vikao vyote vya kaunti hiyo wakilalamikia mishahara duni na kushindwa kwa serikali kukagua malipo yao.

 

Wawalikishi hao katika utawala wa Gavana Cecily Mbarire wameapa kutofanya kikao chochote hadi lalama zao zisikizwe wakisema hatua yao ya kusitisha vikao hivyo inalingana na maazimio yaliyotolewa Mei 3, 2023, wakati muungano wa wanachama wa mabunge ya kaunti walikutana katika Kituo cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC).

 

Akiwahutubia wanahabari baada ya wanachama hao kuahirisha kikao cha bunge mnamo Jumatano, Mei 31, 2023, Mwakilishiwadi wa Mbeti Kusini Murithi Kiura alisema walikuwa wakipokea Ksh123,000 kama mshahara wao lakini sasa imeshuka hadi Ksh86,000. akisema wana majukumu zaidi ya kutekeleza.

 

Viongozi hao pia wanashinikiza Hazina ya Maendeleo ya Wadi NG-CDF na Hazina ya Utekelezaji wa Haki za Kaunti kwa Wanachama walioteuliwa wa Bunge la Kaunti.

 

Hoja hiyo ambayo ilitolewa na mwakilishiwadi Lenny Masters wa Kiambere wakati uo huo inataka kurejeshwa kwa malipo ya marupurupu ya matumizi kwa Wawakilishi wa Wadi wanaotoka maeneo ya mbali katika eneo la ndani la kaunti pamoja na marupurupu ya vikao.

 

Mjumbe wa bunge la kaunti Mumenji Newton Karis akiunga mkono hoja hiyo alisema kuwa kusitishwa kwa vikao hivyo kutafungua milango kwa mashauriano zaidi na afisi mbalimbali zinazohusika ili kupata suluhu la amani la lalama zao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!