Home » Malala: Jinsi Ruto Alivyokabiliana Na Makataa Ya Raila

Katibu Mkuu wa United Democratic Alliance (UDA), Cleophas Malala amefichua jinsi Rais William Ruto alivyokabiliana na makataa ya Azimio iliiyopa serikali hadi usiku wa manane Jumanne, Mei 30 kutekeleza.

 

Azimio ilikuwa ameupa muungano wa Kenya Kwanza masharti matatu kabla ya kurejea kwenye mazungumzo ya pande mbili.

 

Akizungumza wakati wa mahojiano na runinga moja humu nchini, Malala amefichua kuwa Rais amechagua kupuuza kabisa madai yaliyotolewa na Azimio na kuzingatia mamlaka yake.

 

Malala ameonya kuwa Serikali haiwezi kuchukua maagizo wala kusalimisha matakwa ya upinzani.

 

Seneta huyo wa zamani wa Kakamega amekerwa na kauli za Azimio kwa rais akionyesha kwamba vitisho vya upinzani kwa sasa vimezoeleka.

 

Madai ya azimio ambayo ilitaka kutekelezwa kabla ya usiku saa sita Jumanne ni pamoja na kuondolewa kwa Mswada wa Fedha 2023, Kenya Kwanza kutoingilia vyama tanzu vya Azimio haswaa Jubilee, na kushughulikia kupanda kwa gharama ya maisha.

 

Azimio ilitaka Mswada wa Fedha uondolewe na nafasi yake kuchukuliwa na pendekezo linalotambua malalamiko ya wananchi.
Upinzani unatarajiwa kurejelea maandamano ya nchi nzima ili kumshinikiza Rais William Ruto.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!