Migori: Mwanaume Wa Miaka 23 Apigwa Hadi Kufa

Mwanamume mwenye umri wa miaka 23 amefariki katika nyumba inayoshukiwa kuwa nyumba ya mjane katika kijiji cha Lidha, eneo la West Kadem, kaunti ndogo ya Nyatike.
Kulingana na chifu wa eneo hilo .Clime Malongo, marehemu aliyetambulika kama Polycap Ochola alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34.
Katika usiku huo wa maafa, inasemekana alienda nyumbani kwa mwanamke huyo na kushambuliwa na mwanamume mwingine, ambaye pia anashukiwa kuwa na uhusiano na mwanamke huyo.
Kulingana na .Malongo, wanaume hao wawili walipigana dhidi ya mwanamke huyo, na kuvutia hisia za majirani, ambao pia walifika kushuhudia pambano hilo.
Amedai kuwa mpenzi wa mjane huyo, Polycarp Ochola, alipigwa hadi kufa na umati wenye gadhabu.
Wakati uo huo, familia ya marehemu, katika shambulio la kulipiza kisasi, iliteketeza nyumba tatu nyumbani za mjane huyo.
Chifu wa eneo hilo pia amesema kuwa watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha mwanaume huyo wametiwa nguvuni.
Kulingana na wakazi tukio hilo limesababisha msuguano kati ya familia ya mjane na familia ya marehemu.
Chifu ametoa wito kwa jamii kuwapa muda polisi kuchunguza suala hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe.