Home » Mbosso Azungumzia Kifo

Mwimbaji wa Tanzania Mbosso anasema kifo ni ukumbusho wa uwepo wa Mungu katika maisha yetu.

 

Msanii huyo wa nyimbo ya ‘Hodari’ alikuwa akijibu alipoulizwa kuhusu kifo cha rafiki yake kutoka Afrika Kusini, mwimbaji wa Amapiano Costa Titch.

 

“Hatukupata nafasi ya kufanya collabo nyingine baada ya ‘Moyo’ na ‘shetani,” aliiambia Wasafi Media.

 

Akiongeza “Kifo ni ukumbusho wa uwepo wa Mungu katika maisha yetu. Leo ni yeye, kesho ni mimi na siku nyingine ni mtu mwingine.”
Kwa hivyo maoni yake ni nini juu ya kifo?

 

“Kila mtu atapita kwa sababu imeandikwa kila mtu ataonja mauti. Hatuwezi kukwepa, inabidi tujiandae, kuishi vizuri na watu, kuhakikisha unaacha urithi mzuri duniani.”

 

Aliwataka wafuasi wake kuendelea kusali katika dini yoyote waliyomo.

 

“Kifo Kipo.”

 

“Kwangu mimi ilikuwa ni ukumbusho kuwa kifo kipo, alikufa akiwa anatumbuiza, unaweza kufa ukiwa kwenye usaili au ukifanya chochote. Mungu anaweza kukuchukua muda wowote na huu ni ukumbusho kwamba tutamrudia Mungu.”

 

Alihimiza;

 

“Hakuna aliyewahi kwenda na kurudi na kutuambia jinsi ilivyo huko. Mungu aliweka siri lakini imani yetu itatuokoa.”

 

Mbosso na Costa Titch walifanya kolabo mbili kabla ya kifo chake. Titch alifariki alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la muziki la Ultra mjini Johannesburg.

 

Familia yake ilimzikaa Marchi 15 katika hafla ya maziko ya kibinafsi.

 

“Kama familia tunakabiliwa na wakati mgumu tunapojaribu kuelewa kile kilichotupata,” ilisoma taarifa ya familia.

 

Familia iliomba zaidi ipewe muda na nafasi ya kujikusanya “Familia ya Tsobanoglou inawashukuru kwa upendo na msaada mliompa mtoto wetu na muendelee kumuinua hata kiroho. Tunaomba utuweke katika maombi na kuinuliwa katika Bwana.”

 

Katika taarifa nyingine, familia iliwashukuru marafiki na mashabiki kwa kuendelea kumpenda na kumuunga mkono marehemu mtoto wao.

 

“Tulimuaga mtoto wetu, kaka na rafiki yetu Jumatano Machi 15, katika hafla ya faragha iliyozungukwa na familia ya karibu na upendo mwingi,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

 

“Familia ya Tsobanogou ingependa kutoa shukrani nyingi kwa jumuiya ya Titch Gang duniani kote kwa upendo wao endelevu na usaidizi katika wakati huu mgumu sana.”

 

“Kuwa na nyinyi nyote kushiriki video, picha na kumbukumbu ambazo mtoto wetu alikuwa nazo kwa wengi kumepunguza maumivu tunayobeba.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!