Home » Wataalamu Wafanyia Uchunguzi Miili 34 Ya Shakahola

Uchunguzi wa maiti uliofanywa hiyo jana Jumatatu kwa waathiriwa 22 wa Shakahola katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi haukuweza kubaini chanzo hasa cha kifo.

 

Mwanapatholojia mkuu wa Serikali Johansen Oduor, alisema miili hiyo ilikuwa imeharibika vibaya kiasi cha kutotambulika.

 

Akihutubia wanahabari, Odor alisema kufikia sasa wameifanyia uchunguzi miili 34 wakiwemo watoto 12.

 

Hii inafikisha 79 idadi ya uchunguzi wa miili iliyofanyika tangu awamu ya pili ya zoezi la waathiriwa 129 kuanza tena wiki iliyopita.

 

Kati ya hao 34 walikuwa wanawake 21 na wanaume 10 pamoja na watatu ambao jinsia yao haikuweza kujulikana.

 

Oduor Alisema timu hiyo ambayo ilikuwa imepumzika mwishoni mwa wiki kutokana na uchovu, haikuweza kubaini sababu za vifo vya miili 20 kati ya hao huku kumi na mbili ikionyesha dalili za njaa.

 

Kiongozi wa madhehebu hayo Paul Makenzi wa Kanisa la Good News International ambaye bado anazuiliwa na polisi anasemekana kuwashawishi wafuasi wake kufa kwa njaa.

 

Kuna uwezekano kuwa zoezi la uchunguzi wa maiti linaweza kumalizika wiki hii, na hivyo kufungua njia ya kuanzishwa upya kwa ufukuzi wa miili ndani ya shamba la ekari 800 la Mackenzie huko Shakahola, ambalo Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alisimamisha wiki iliyopita.

 

Kindiki alisema bado kuna makaburi mengi zaidi kwenye shamba hilo, yakiwemo makaburi ya pamoja yapatayo 10 ambayo tayari yametambuliwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!