Home » ODM Yamtimua Naibu Gavana Wa Siaya William Oduol

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM kimemtimua Naibu Gavana wa Siaya William Oduol kutoka chama hicho.

 

Uamuzi huo uliwasilishwa na kamati ya uratibu ya ODM Siaya kutoka kaunti zote ndogo.

 

Chama hicho kwenye taarifa kimefichua kuwa sababu ya kumfukuza naibu wa Gavana James Orengo ni kwa sababu alikuwa akifanya kazi na Kenya Kwanza.

 

Kamati hiyo pia ilifanya mabadiliko kwa uongozi wa chama cha Gem na Bondo, ikishikilia kuwa watu hao hawatatambuliwa tena kuwa wanachama wa ODM.

 

ODM iliibua wasiwasi kwamba Kenya Kwanza ilikuwa ikitumia msaada wa chakula kuwarai wanachama kujiunga na muungano wao.

 

Oduol ametimuliwa siku mbili baada ya kutoa madai ya ubadhirifu wa kifedha dhidi ya Gavana James Orengo na wanachama wengine wa bunge la kaunti.

 

Wakati wa mahojiano na vyombo vya habari, Oduol aliyezingirwa na wapinzani wake alidai kuwa kaunti ilitoa hadi Ksh6 milioni kwa siku.

 

“Kwa siku moja, mfanyakazi mmoja mdogo hutumwa kwa benki mara sita hadi nane, akitoa Ksh950,000 kila wakati. Hii ni kukwepa matakwa ya benki kuu ya Kenya CBK kwenda na hati wakati wa kutoa Ksh1 milioni,” alidai.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!