Home » Homa Bay: Binti Mmoja Anajisiwa Na Wanaume Sita

Familia moja katika eneo bunge la Ndhiwa, Kaunti ya Homa Bay, inatafuta haki kwa binti yao mwenye umri wa miaka 17 anayedaiwa kunajisiwa na kundi la wanaume sita.

 

Mwathiriwa kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay ambapo alikimbizwa akiwa na majeraha baada ya kisa hicho kilichotokea Jumatatu usiku katika Mji wa Homa Bay.

 

Kulingana na familia yake, msichana huyo aliondoka nyumbani kwa Ndhiwa wiki mbili zilizopita na mamake hakujua alikokwenda.

 

Msichana huyo amesema wanaume hao walimkabili walipokuwa wakitembea katika Mji wa Homa Bay usiku na kumnajisi karibu na kituo Fulani cha pombe.

 

Baada ya tukio hilo, alisema mmoja wa wanaume hao alijaribu kulazimisha kuingiza tindikali (acid) kwenye sehemu zake za siri, kabla ya baadaye kuripotiwa kumpeleka sehemu tofauti.

 

Afisa wa watoto katika kaunti ndogo ya Homa Bay Joseph Otieno amesema amepokea habari kuhusu kisa hicho na afisi yake inashirikiana na maafisa wa usalama kuwatafuta washukiwa hao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!