Home » Fantana Aeleza Kwa Nini Alimbusu Diamond Platnumz Kwenye TV

Fantana Aeleza Kwa Nini Alimbusu Diamond Platnumz Kwenye TV

Mwimbaji na mwigizaji wa Ghana Fantana amekuwa akigonga vichwa habari baada ya yeye na Diamond Platnumz kubusiana kwenye reality show ya Netflix Young, Famous, and African.

 

Wawili hao walibusiana na kutembea ghorofani ‘kumaliza shughuli zao.’

 

“Tulibusiana na tukapanda ghorofani, chochote kilichotokea, kilifanyika,” alisema katika mazungumzo ya hivi majuzi na mwigizaji mwenzake Khanyi Mbau.

 

Alipoulizwa kwanini alimbusu mwimbaji huyo wa Tanzania, Fantana alisema;

 

“Diamond anavutia.”

 

Fantana pia alifichua kuwa anahisi ni muhimu kufanya mapenzi katika tarehe ya kwanza “Kwa nini uendelee kusubiri kwa wiki mbili? Hata siku mbili ni ndefu sana. Na kisha ujue baadaye kwamba huwezi.”

 

Katika shoo hiyo, Diamond alikataa kukiri kuwa anatoka kimapenzi na mwimbaji Zuchu. Fantana anasema anaamini mwimbaji huyo yuko sokoni kwa sababu alimwambia kuwa alikuwa hajaoa.

 

“Ikiwa una rafiki wa kike na ukasema hapana, ninakubali neno lako. Sipendi kuhangaika na wanaume wenye marafiki wa kike.”

 

Katika shoo hiyo, Fantana aligombana vikali na Zari the Boss lady baada ya mwimbaji huyo wa Ghana kumtuhumu Zari kuwa ana mapenzi na babake watoto.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!