Home » SRC Yaokoa Wakenya

Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) imefichua kwamba imeidhinisha maombi ya thamani ya Ksh411 milioni dhidi ya maombi 65 kutoka kwa taasisi za umma ya jumla ya Ksh3.2 bilioni.

 

Aidha katika hatua hiyo,sasa imebainika kwamba SRC iliokoa wakenya kutoka kwa Ksh2.8 bilioni, sawa na asilimia 12.7 ya maombi yote.

 

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, SRC imesema ilipokea maombi 65 kutoka kwa taasisi za umma kati ya Januari hadi Machi 2023, kwa mwaka wa kifedha wa 2022-2023.

 

Tume hiyo pia imeeleza kuwa gharama ya jumla ya maombi ya taasisi za umma kwa robo tatu ya Mwaka wa Fedha (FY) 2022/2023 ni Ksh5.9 bilioni, ikilinganishwa na Ksh18.8 bilioni katika kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2021/2022.

 

Wakati uo huo, SRC imebaini kuwa matumizi ya Mapato ya Wafanyakazi (P.E) katika serikali za kaunti yalisalia juu ya kiwango cha Usimamizi wa Fedha za Umma (P.F.M).

 

Kulingana na Ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti (OCOB), jumla ya matumizi ya P.E katika serikali za kaunti yalitarajiwa kuongezeka kutoka Ksh90.4 bilioni katika robo ya pili hadi Ksh126.02 bilioni katika robo ya tatu.

 

SRC imeonyesha kuwa bili ya mishahara kwa uwiano wa kawaida wa Pato la Taifa (G.D.P) ilikuwa asilimia 7.91 katika Mwaka wa Fedha wa 2016/2017, na kupanda hadi asilimia 8.82 katika Mwaka wa Fedha wa 2019/2020.

 

Uwiano ulipungua hadi asilimia 8.25 katika Mwaka wa Fedha wa 2020/2021 na ilitarajiwa kupungua zaidi hadi asilimia 7.73 katika Mwaka wa Fedha wa 2021/2022.

 

Kadhalika , SRC ilikadiria uwiano huu kupungua hadi asilimia 7.5, kulingana na wastani wa nchi zinazoendelea, na takriban asilimia 7, kiwango kinachohitajika kimataifa.

 

Pato Halisi la Ndani (G.D.P) liliongezeka kwa asilimia 4.8 mwaka 2022, ikilinganishwa na ukuaji uliofanyiwa marekebisho wa asilimia 7.6 mwaka 2021.

 

Zaidi ya hayo, SRC imebainisha kuwa uchumi wa Kenya ulitarajiwa kukua kwa asilimia 6.1 mwaka wa 2023 na kudumisha kasi hiyo katika muda wa wastani.

 

Kulingana na tume hiyo, ukaguzi wa Utafiti wa Kiuchumi wa 2023 unaonyesha jumla ya wafanyikazi wa Kenya walikuwa milioni 12.

 

Kati ya hizo, milioni 2 zinaunda sekta rasmi, ikijumuisha utumishi wa serikali, mashirika ya umma na wafanyikazi wa sekta binafsi.

 

Watumishi wa umma waliongezeka kutoka 774,700 mwaka 2015/2016 hadi 923,100 katika Mwaka wa Fedha wa 2020/2021.

 

Kwa wastani, nguvu kazi ya utumishi wa umma ilikua kwa asilimia 4.34 kufikia Mwaka wa Fedha wa 2020/2021 na ilitarajiwa kukua kwa kiwango sawa na wafanyakazi 963,200 katika Mwaka wa Fedha wa 2021/2022.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!