Home » Ole Sapit Kwa Ruto: Ahadi Zako Nyingi Hazikuwa Za Uhalisia Kubali

Ole Sapit Kwa Ruto: Ahadi Zako Nyingi Hazikuwa Za Uhalisia Kubali

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Kenya Jackson Ole Sapit amemrai Rais William Ruto kukubali kwamba ahadi zake za kampeni za 2022 hazikuwa za kweli.

 

Sapit amemuonya rais ruto kuwa anaweza kupoteza imani ya Wakenya katika maneno yake ikiwa ataendelea kutoa ahadi bila kutimiza zile za dharura zaidi.

 

Ole Sapit ameeleza kuwa Ruto anaweza kuweka shinikizo nyingi kwa taifa kwa kujaribu kuonekana tofauti na asili ya wanasiasa kote ulimwenguni.

 

Aidha Onyo la Sapit linajiri wakati serikali ya Kenya Kwanza ilikuwa chini ya shinikizo la kutimiza ahadi huku kukiwa na hali ngumu ya uchumi ambayo ilishuhudia bei ya bidhaa muhimu ikipanda juu.

 

Kwa mfano, hazina ya nyumba, ambayo inakaribia kuwa sheria, imesababisha shutuma nyingi miongoni mwa Wakenya kote nchini.

 

Ahadi kuu za Rais Ruto katika uchaguzi wa wagombea Urais wa Agosti 2022 zilijumuisha kupunguzwa kwa gharama ya maisha katika siku 100 za kwanza ofisini.

 

Ruto alieleza kuwa atawekeza kwenye kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula mashinani ili kuunda mfumo wa ziada ambao utashuhudia bei ya bidhaa kushuka.

 

Ili kufanikisha hili, utawala wa Ruto uliidhinisha ruzuku ya mbolea iliyoruhusu wakulima kununua mfuko wa kilo 50 kwa Ksh3,500 kutoka zaidi ya Ksh6,000. Rais alisema kuwa mbinu hiyo ingependelea gharama ya uzalishaji na kuongeza mavuno.

 

Rais Ruto pia aliahidi kuunda nafasi za kazi milioni moja kwa vijana kwa mwaka kwa kuwekeza katika viwanda na miundomsingi, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Nyumba za Nafuu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!