Home » Kenya Kwanza Yaishtumu Azimio

Timu ya mazungumzo ya pande mbili ya Kenya ya Kwanza imemshutumu wenzao wa Azimio kwa kuweka vizuizi visivyo vya lazima katika juhudi za kuwa na mazungumzo yenye tija.

 

Timu hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wao George Murugara wamedai Azimio inatafuta visingizio vya kutatiza mazungumzo hayo.

 

Murugara amesema kuna masuala ya dharura kama vile tume Huru ya mipaka IEBC ambayo haiwezi kuzuiwa kwa muda mrefu sana.

 

Kulingana naye atamwandikia mwenyekiti wake Otiende Amollo ambaye alimshutumu kwa kusimamisha mazungumzo kabla ya wakati wake rasmi.

 

Murugara anasema atamwomba mwenyekiti mwenza kufanya mazungumzo ili kusuluhisha maswala ambayo hayajakamilika kabla ya kurejelea mazungumzo na makataa ya Azimio Jumanne wiki ijayo.

 

Kutokana na hofu kuwa kamati hiyo huenda ikapitwa na wakati kabla ya kukubaliana na lolote, Murugara amesema wana kipengele katika mwafaka wa makubaliano ya kuongeza muda ikihitajika.

 

Azimio iliahirisha mazungumzo hayo siku ya Jumanne ikiwashutumu wenzao kwa ukosefu wa maelewano kwa baadhi ya masuala ambayo walitaka kujadiliwa kwanza na kuafikiana kabla ya kutoa ripoti kamili muda utakapofika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!