Seneta Orwoba Azungumza Kuhusu Nguo Ya Doa
Seneta mteule Gloria Orwaba amepongeza maendeleo yaliyopatikana katika masuala ya hedhi nchini Kenya kabla ya siku ya usafi wa hedhi ambayo itaadhimishwa duniani kote Mei 28.
Seneta huyo alisimulia uzoefu wake wa kibinafsi, ambapo aliingia katika majengo ya bunge akiwa na nguo iliyotiwa rangi mnamo Februari 15, 2023 jambo ambalo Maseneta waliibua wasiwasi kuhusu doa la Orwoba na kusababisha Spika Amason Kingi kuamua aondoke bungeni.
Orwoba alizidi kutetea hatua yake kwa misingi kwamba amekuwa akipigania dhidi masuala ya hedhi tangu mwaka 2007 na hali hiyo ilimlazimu kutekeleza yale ambayo amekuwa akiwafundisha wasichana wachanga kuhusu kujithamini wanapokuwa kwenye vipindi vyao vya hedhi.
Vile vile ameelezea umuhimu wa utetezi wa usafi wa hedhi na usawa wa usambazaji wa taulo za usafi, akithibitisha kuwa zote ni muhimu.
Kulingana naye baadhi ya wanawake magerezani wanashiriki taulo moja ya hedhi kutokana na kukosa uhuru wa kujieleza na kupata pedi.
Orwoba amechora taswira ya jamii nchini Kenya ambapo mwanamke haruhusiwi kuingia katika kila sehemu katika siku zake za hedhi.