Home » Rais Ruto Aongoza Mkutano Wa Wabunge Wa Kenya Kwanza Ikulu

Rais Ruto Aongoza Mkutano Wa Wabunge Wa Kenya Kwanza Ikulu

Rais William Ruto ameongoza mkutano wa kundi la wabunge katika Ikulu leo, Jumanne, Mei 23.

 

Wabunge na viongozi wengine wa serikali wakiwemo Mawaziri wamehudhuria mkutano huo, kulingana na picha zilizoonekana mitandaoni .

 

Baadhi ya wajumbe mashuhuri walioonekana ni waziri wa teknolojia na mawasilaino ICT Eliud Owalo, Waziri wa Mazingira Soipan Tuya, Seneta Mteule Veronica Maina na Mbunge wa Mugirango Kusini ,Kinara wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Sylvanus Osoro.

 

Wabunge wa chama cha Jubilee ambao wamekuwa wakiunga mkono Kenya Kwanza, akiwemo Sabina Chege na Adan Keynan pia wamehudhuria.

 

Rais Ruto alikuwa amedokeza awali kuwa miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni jinsi vituo vya teknolojia vitasambazwa katika kila eneo kote nchini ili kuimarisha upatikanaji wa ajira za kidijitali.

 

“Lazima tuwe na nia ya kuunda nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana. Nitafanya mkutano na viongozi Jumanne tunakubaliana jinsi tutakavyounda vituo vya ICT katika kila wadi nchini Kenya ili tuwape vijana wetu kazi za kidijitali,” alisema wakati wa ibada ya shukrani huko Isiolo siku ya Jumapili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!