Home » Lukresia Robai Atua Kwenye Tamasha La WHO Uswizi

Lukresia Robai, mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Matibabu cha Kenya (KMTC) ambaye alipata umaarufu kwa kuwachezea wagonjwa wake katika wadi za hospitali na kushiriki kwenye Tiktok, ameona milango yake ikifunguliwa zaidi.

 

Robai kwa mara nyingine amekuwa gumzo baada ya kipande cha video kusambazwa mtandaoni, kikimwaonyesha  akiwaburudisha wageni wake nchini Uswizi.

 

Muuguzi huyo anayeishi Kitale alikuwa mmoja wa walioalikwa kuwaburudisha waliohudhuria katika hafla ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ‘Walk the Talk’ mjini Geneva.

 

Katika video hiyo, wimbo maarufu wa ‘Mkono wa Bwana’ wa Zablon Singers wa Tanzania unavuma kwa mfumo wa sauti, huku Robai akiwaongoza wasanii wa densi kuwaburudisha mamia ya watu waliohudhuria hafla hiyo.

 

Miondoko yake iliwavutia waliohudhuria ambao pia walijiunga kwenye densi hiyo.

 

Billy O’clock ilimfikia kuhusu uzoefu huko Geneva, na akasema: “Nilialikwa na Shirika la Afya Ulimwenguni kushiriki katika maongezi ya afya kwa wote Uzoefu wangu kwenye hafla hiyo umekuwa mzuri”.

 

Robai alisisimua mtandaoni wakati video zake akicheza na watoto katika hospitali ya Kitale level four ziliwashangaza watazamaji.

 

Lengo la tukio la ‘Walk the Talk’ “ni kukuza umuhimu wa mitindo ya maisha yenye afya, kuongeza ufahamu juu ya kufuatilia afya kwa wote, na kusherehekea umuhimu wa ushirikiano.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!